|
|
|
![]() ![]() |
![]() |
|
Study The Bible
|
http://ktn2.netfirms.com WorldSpace
Hawajui Wamlenge Nani Wanatumia setilaiti kurusha matangazo ya redio pamoja kurasa za "Internet" walizochagua wao, cha ajabu ni kwamba wanataka watu walipe ili waweze kupokea matangazo ya redio ambayo yamekuwa yakipokelewa bure tangu nishati ya redio ianze. Wale ambao wangenufaika zaidi na huduma yao ni watu wa mashambani ambako FM nyingi za mijini haziwafikii. Lakini bei za vyombo vya kupokea matangazo hayo kutoka "Setilaiti" ni ghali mno kiasi kwamba watu wa mashambani hawawezi kumudu. Siyo hivyo tu, malipo ya kila mwezi yanawafanya wawe hawataki kusikia kitu kinachoitwa WorldSpace. Nao wakazi wa kima cha chini mijini hawana hitaji la WorldSpace kwani FM nyingi zilizoko hewani zinakithi mahitaji yao yote ya redio. Isitoshe wanatumia redio za bei ya chini kupokea FM zote. Ni ukweli usiopingika kwamba siku hizi ukiwa na Kshs 200 unajipatia redio nzuri kabisa inayoweza kushika matangazo ya FM pamoja na SW. Wakazi wa mijini wanaoitwa watu wakima cha kati, hawa ni wale ambao kwa njia moja ama nyingine wanaweza kutumia kompyuta. Aidha ziwe ni zao binafsi,au wanaweza kuzikodi kwa muda wakaingia kwenye Internet wakaenda wanakotaka na wakatuma ujumbe wanakotaka kisha mahitaji yao ya kompyuta siku hiyo yakawa yameisha. WorldSpace wanasema hawa walengwa wao. Eti wanunue "Dekoda" Ksh.9000 halafu kila mwezi walipe kiasi fulani cha pesa, na mwisho wa mambo yote wachaguliwe 'Sait" za kutembelea kwenye Internet. Na unajua ni nani anayewachagulia waende wapi kwenye mtandao? ni WorldSpace. Mbaya zaidi wanatakiwa wakubaliane na chochote watakachokisoma huko.Hawana ruhusa ya kutuma ujumbe kupinga au kukubaliana na walichokisoma huko. Internet
ilikuja kututoa katika utumwa wa kupokea habari bila kutuma
habari, na WorldSpace wanataka kuturudisha utumwani. Tumekataa
haturudi utumwani tena. Wakitaka waitumie teknolojia ya setlait
kutuunganisha na internet na watuache huko. Tuende tunakotaka,
na tutume habari kwa yeyote duniani bila wao kuwa kiranja
wa Internet. Wapunguze bei ya redio zao za setilait ili watu
wamashambani waweze kumudu. Hapo watakuwa wameifanyia Afrika
kitu cha maana sana. kwani mawasiliano yanaweza yakainua kiwango
cha maisha ya waafrika kwa haraka sana. Swaleh Mdoe Anyamazishwa KTN Alipoingia Nairobi akiitangazia Nation TV Alin'gara kama nyota, kila mtu alizungumza kuhusu Swale Mdoe. alipojiunga na KTN alikatwa makali kwa kunyamazishwa bila kusoma habari.Anaweza akawa analipwa mshahara mkubwa kuliko Nation, lakini kitaaluma amekwamishwa. Pengine KTN wanafanya hivyo makusudi ili kumkata makali Swaleh Mdoe.Swali ambalo wengi wanajiuliza ni kama Mdoe anajua haya au anafurahia kuitwa majina makubwa na kuingalia taaluma yake ikiota kutu
|
|
|||||||||||